"Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA – Saeed Ohadi, Naibu wa Rais na Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Shahidi Ayatollah Sayyid Ebrahim Raisi na mashujaa wengine wa huduma, leo asubuhi ya Jumatatu katika mkutano na waandishi wa habari wa Baraza la Uratibu wa Matangazo ya Kiislamu, alitangaza mipango mikubwa na ya kitaifa kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa Shahidi kwa Mashahidi hao."
Ohadi, akimkumbuka na kumheshimu shahidi pamoja na mashujaa wa huduma, alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho si tu kufanya hafla ya kawaida, bali ni hatua ya kina na ya kimkakati.
Alieleza kuwa baada ya agizo la Rais, kwa mujibu wa Baraza la Uratibu wa Matangazo ya Kiislamu na kwa amri ya Bwana Musipour, Kamati hiyo iliundwa kwa mtazamo wa kina zaidi juu ya tukio hili.
Akizungumzia kuhusu kuitwa kwa tukio hili kama “Wiki ya Huduma”, alisema:
Katika kalenda rasmi ya nchi kuna matukio mbalimbali, lakini hadi sasa hakukuwa na wiki iliyotengwa kwa jina la “huduma”. Wiki hii ni fursa ya kuwatukuza mashujaa waliotoa maisha yao kwa ajili ya kuwahudumia watu.
Kwa mujibu wa Ohadi, zaidi ya taasisi na mashirika 40 yameshiriki kikamilifu katika vikao vya kamati kuu, na muundo wa shughuli umeundwa kwa kamati sita maalum: uenezi wa habari, masuala ya kimataifa, matangazo ya mijini, kitamaduni na kisanii, ushiriki wa wananchi, na maudhui.
Naibu Rais alibainisha kuwa sifa ya pamoja ya mashahidi wote wa huduma ni kuwa walikuwa watu wa watu, na akaeleza kuwa:
Hafla za maadhimisho zinapaswa kuwa za umma ili kukuza utamaduni wa kujitolea na huduma ndani ya jamii kwa kushirikisha watu moja kwa moja.
Akielezea kujitolea kwa Ayatollah Raisi, Ohadi alisema kuwa kutokana na roho ya kujitolea ya Rais aliyekufa shahidi, hafla ya kuwakumbuka mashujaa wote wa huduma itafanyika kwa pamoja.
Pia alieleza kuwa mipango hiyo imegawanywa katika maeneo makuu matano, na kuongeza kuwa:
Vikundi vya kujitolea na kamati za wananchi kote nchini, kutoka mijini hadi vijijini, vitafanya zaidi ya maonyesho ya kusafiri 15,000, kutuma makundi ya kujitolea kwenda maeneo yenye mahitaji, kufanya maigizo ya mitaani na hafla kwenye makaburi ya mashujaa. Jumla ya huduma zaidi ya milioni 7 zitolewa na mashirika wakati huu.
Kuhusu majina ya Siku za Wiki ya Huduma, alisema:
Siku moja itaitwa "Juhudi na Kutokuchoka", nyingine "Huduma na Kuondoa Umaskini", na nyingine "Diplomasia ya Muqawamah", ili kuonyesha nyanja mbalimbali za huduma ya mashujaa.
Aliongeza kuwa:
Kwa mtazamo wa muda mrefu, tunatarajia wiki hii kuwa mwanzo wa mchakato wa kuanzisha harakati ya kiutamaduni kwa ajili ya kueneza utamaduni wa huduma miongoni mwa kizazi kijacho.
Ohadi alitangaza kuwa:
Katika wiki hii, shule 110 zitafunguliwa na vikosi vya Basiji na raia wa kawaida, na pia "meza elfu moja za huduma" zitaandaliwa katika Swala za Ijumaa kote nchini, kwa ushiriki wa mahakama.
Kwenye nyanja ya utamaduni na vyombo vya habari, Ohadi alisema kuwa video fupi 22 (klipu au nyimbo za kisanii) zimetengenezwa na taasisi ya Sanaa ya Kiislamu na zitapeperushwa kupitia televisheni ya taifa (Seda va Sima).
Aidha, filamu 12 za makala ziko tayari kuonyeshwa, zikiwemo:
-
"Bwana Mwanadiplomasia" kuhusu Shahidi Amir-Abdollahian,
-
"Kuruka Katika Ukungu",
-
"Taarifa ya Rais Aliyekufa Shahidi",
-
Na Filamu Makala (Documentary) ya: "Kutokea Ghafla (Sar-zadeh)".
Naibu Rais alieleza pia kuwa kwa agizo la Rais, Magavana wa mikoa wataongoza kamati za mikoa ili kuhakikisha kwamba shughuli za maadhimisho zinafanyika kwa nguvu kote nchini. Hasa katika mikoa ya asili au ya utumishi wa mashujaa wa huduma, programu maalum zimepangwa.
Kuhusu ratiba ya shughuli, Mkuu wa Kamati ya Maadhimisho aliongeza:
Siku ya Alhamisi, mkutano wa kitaifa wa kuwakumbuka mashujaa wa huduma utafanyika kote nchini. Jijini Tehran, hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Imam Hussein (a.s.) na itahutubiwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (IRGC), Jenerali Hussein Salami.
Siku ya Ijumaa, wanachama wa serikali ya kumi na tatu na ya kumi na nne watahutubia katika sala za Ijumaa kote nchini.
Pia alitangaza kufanyika kwa mikutano sita ya kisayansi katika Chuo Kikuu cha Tehran, akisema kuwa:
Mkutano maalum kuhusu "Diplomasia ya Mshikamano" pamoja na kongamano la kimataifa kuhusu mada hiyo, yatakayohutubiwa na Rais Dkt. Pezeshkian na Hujjatul-Islam Mohseni-Ejei, Mkuu wa Idara ya Mahakama, ni miongoni mwa matukio muhimu ya kielimu katika Wiki ya Huduma.
Pia, kwa mnasaba wa usiku wa shahada, symphony ya kifahari ya vipengele vitano iitwayo "Hadithi ya Symphony ya Mei" itatumbuizwa kwa mara ya kwanza, na Dkt. Qalibaf atakuwa mzungumzaji katika hafla hii.
Mkuu wa Kamati ya Maadhimisho ya Mashahidi wa Huduma, mwishowe alitoa shukrani kwa ushirikiano wa familia za Mashahidi wa huduma, Mashirika ya kijamii, na Serikali ya kumi na nne, na alieleza matumaini yake kwamba hafla hii itakuwa mwanzo wa msimu mpya katika kuenzi hadhi ya wateule halisi wa taifa.
Your Comment